Skip to main content

Posts

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakagua Mradi wa WHC iliyopo Kigamboni

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing (WHC), Dk Fred Msemwa akifafanua jambo wakati  akitoa maelezo kwa  Kamati ya Bunge ya  Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati ilipotembelea na kukagua miradi ya WHC iliyopo Kigamboni Gezaulole na Bunju jijini Dar es salaam. Kamati ya Bunge ya  Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakikagua Mradi wa WHC iliyopo  Kigamboni Gezaulole jijini Dar es Salaam. Baadhi ya nyumba za WHC zilizopo Kigamboni Gezaulole jijini Dar es Salaam.  Miradi ya WHC iliyopo B unju B jijini Dar es Salaam.  Dar es Salaam. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeitaka Taasisi ya Watumishi Housing (WHC) kuendelea kuwa wabunifu wa kijenga nyumba na kuuza gharama nafuu na kutoa muda wa miaka 25 kwa mkopaji ili aweze kulipa deni lake. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati kamati hiyo ikifanya ziara ya kukagua miradi ya WHC iliyopo Gezaulole Kigamboni pamoja na Bunju B, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge na Hesabu za Ser
Recent posts

Makampuni ya simu za mkpononi nchini yameridhia kuunda mifumo wezeshi

Makampuni ya simu za mkpononi nchini Tanzania yameridhia kuunda mifumo wezeshi itakayo wawezesha wananchi wanaotumia hidima za smu kupata taarifa mbalimbali za ujasiriamali, biashara, afya na elimu suala ambalo litachochea upatikanaji wa ajira na kukuza kipato. Makubaliano hayo yanafuatia ripoti ya utafiti ilitolewa leo Jijini Dar es salaam, utafiti uliofanywa na taasisi za REPOA, DTBI,TPSF kuusu namna ambavyo makampuni ya simu za mkononi yanavyoweza kuchochea ukuaji wa shuguli za kiuchumi na hata kuliwezesha taifa kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo mwaka 2015. Msimamizi wa utafiti huo, Dk. George Mulamula kutoka DTBI amesema tafiti inaonyesha  uwezo mkubwa ambao ukitumika na makampuni hayo utawezesha taifa kukuza ajira hususan kwa wanawake na vijana huku wakizingazia namna ambavyo watawafikia watu wa vijijini.

KAMATI YA KUDUMU YA MIUNDOMBINU YATOA NENO KWA WIZARA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupeleka fedha kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Mtwara - Newala - Masasi (KM 210), sehemu ya Mtwara - Mnivata yenye urefu wa KM 50 ili kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo. Kamati hiyo imeonesha kutokuridhishwa na kasi ya mradi huo ambao mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 47 kwa sababu changamoto ya fedha kutolipwa kwa wakati. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, amezungumza hayo wakati wa majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa miundombinu mkoani Mtwara jana ambapo walitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unaojengwa na mkandarasi Dott Services kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 89. "Kama kamati sijaridhishwa na maendeleo ya mradi huu na sababu kubwa ya kucheleweshwa imesemwa hapa ni kuchelewa kwa malipo ya mradi huu, hali hii itachelewesha maendeleo katika mikoa hii hivyo Wizara mjitahidi fedha zije ili mradi ukam

Spika Job Ndugai afanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge alipomtembelea leo tarehe 19 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu wa Spika, Said Yakubu na kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka  Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (katikati) alipomtembelea leo tarehe 19 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka  Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akifurahi jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka nje ya Ofisi ya Bunge leo tarehe 19 Machi, 2019 Jijini Dodoma.  Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akifurahi jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka (kulia) nje ya Ofisi ya Bunge leo tarehe 19 Machi, 2019 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge Spika wa Bunge,